GAVANA KINGI NA RAILA WATOFAUTIANA HADHARANI

Gavana wa kaunti ya Kilifi Amason Kingi ametakiwa kusitisha juhudi zake za kuunga mkono swala la kuundwa kwa chama cha kisiasa, kilicho na mizizi yake hapa Pwani kinachodaiwa kuwa na malengo ya kuwaunganisha viongozi wa Ukanda huu.

Haya ni kwa mujibu wa Kinara wa chama cha ODM Raila Amolo Odinga katika hotuba yake eneo la Cleopatra hapa Malindi ambaye amesema kuwa kwa kipindi kirefu amekuwa akimuunga mkono gavana huyo na ni wajibu wa Kingi kuunga mkono harakati za za  chama cha ODM na kubadili msimamo wake wa kupigia debe hatua ya kuundwa kwa chama cha Wapwani.

Odinga amemtaja gavana huyo kama mmoja wa viongozi wazalendo katika chama cha ODM hivyo kumtaka kuungana pamoja nae na kuendeleza malengo ya chama hicho.

Aidha kwa upande wake Gavana Kingi amepinga kauli hiyo ya kuungana na kinara wa ODM na kuonekana kushikilia msimamo wake wa kuteua kiongozi atakayewania wadhifa wa urais kupitia tiketi ya chama kitakachoundwa cha Pwani.

Kauli ya Kingi imeungwa mkono na mbunge wa Rabai William Kamoti ambaye amehoji ni lazima chama hicho kiundwe ili wapawni wawakilishwe kikamilifu katika nyadhifa za kitaifa.

 

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.