GAVANA KINGI AMSHUTUMU MWANAKANDARSI ANAYEENDELEZA UKARABATI WA BARABARA KUU YA MALINDI – MOMBASA

Gavana wa Kilifi Amason Jeffa Kingi amemshutumu mwanakandarasi anayeendeleza ukarabati wa barabara kuu ya Malindi Mombasa kwa kile alichosema kuwa ameendesha ukarabati huo kwa utepetevu mno.

Akizungumza na wanahabari akiwa katika hospitali ya Tawfiq mjini Malindi kaunti ya Kilifi, Kingi amesema kuwa inasikitisha kuona kwamba barabara hiyo haina alama za barabarani au hata viashiria vya kuonyesha madereva kuwa kuna ukarabati wa barabara unaoendelezwa katika eneo husika.

Kingi ameyasema haya akirejelea ajali iliyotokea mapema hapo jana ambapo watu takribani watu 15 waliripotiwa kufariki dunia kama ilivyokariri idara ya usalama mjini Malindi.

Kingi ameiamuru mamlaka ya ujenzi wa barabara nchini keNHA kuhakikisha kuwa inakamilisha ukarabati wa barabara hiyo hara iwezekanavyo ili kuepuka maafa yanayoshuhudiwa barabarani.

Hatahivyo Kingi amehakikisha kuwa serikali ya kaunti itagharamia matibabu ya majeruhi wote sambamba na kusimamia ada inayotozwa katika hifadhi ya maiti kwa minajili ya wale waliopoteza wapendwa wao.

 

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.