EPL yazuia wachezaji na waamuzi kupeana mikono kabla ya kuanza mechi

Ligi Kuu ya Uingereza wamezuia wachezaji na waamuzi kusalimiana kwa kupeana mikono kuanzia mechi za wikiendi hii hadi watakapopewa taarifa nyingine, hii inakuja kutokana na hofu ya virusi vya korona.

Hatua hiyo inakuja baada ya serikali kuitaka EPL kuimarisha mipango yake ya kujikinga na korona. Timu zitajipanga kama kawaida lakini timu mwenyeji ndio itapita mbele ya timu iliyoikaribisha bila kushikana mikono.

Taarifa za EPL kutangaza hivyo zinakuwa za pili baada ya siku moja nyuma shirikisho la soka Tanzania TFF kutangaza zuio kama hilo kwa wachezaji na waamuzi kutosalimiana kwa kupeana mikono.

Wiki iliyopita meneja wa Newcastle Steve Bruce amesema klabu yake imeacha utaratibu wake wa kupeana mikono wakati wa asubuhi hukubosi wa West Ham David Moyes akisema wachezaji wake watakuwa wakisalimiana kwa kupeana tano badala ya kushikana mikono.

Southampton pia imewapiga marufuku wachezaji wake kutoa saini zao au kupiga selfie na mashabiki.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.