EPL: Wolves yaiburuza Manchester United

Ligi kuu ya Uingereza imefikia patamu, kila timu ikijitahidi kufanya vizuri ili kuwa katika nafasi nzuri zaidi ya kunyakua ubingwa.

Jana zilipigwa mechi mbili, Watford imeifumua Fulham kwa mabao 4-1, nao Manchester United wamekubali kipigo toka kwa Wolverhampton Wanderers cha bao 2-1.

Leo itakuwa zamu ya mechi tatu kuchezwa ikiwemo Manchester City kumenyana na klabu ya Cardiff wakati Spurs ikipimana nguvu na Crystal Palace.

Chelsea yenyewe ikiwa nyumbani itavaana na Brighton.

Mechi zote zimeratibiwa kuanza usiku saa nne kasorobo saa za Afrika Mashariki.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.