EPL | Huenda KDB akakosekana kwenye mechi ya City dhidi ya Arsenal, Guardiola kuzungumza na wanahabari

Pep Guardiola anatarajiwa kuzungumza na waandishi wa habari siku moja kabla ya mechi ya Manchester City ya mitanange ya ligi kuu Uingereza EPL dhidi ya Arsenal.

Guardiola atakuwa na matumiani ya timu kurudi katika fomu yake ya kuandikisha ushindi baada ya kuyumba kwenye mechi ya kuanza kwa msimu mpya wa EPL ambapo imelimwa 5-2 na Leicester City na kutoka sare ya 1-1 dhidi ya Leeds katika mechi mbili za hivi punde.

Aliyekuwa mkufunzi msaidizi wa klabu ya City Mikel Arteta ambaye katika utoaji wa huduma zake kwenye kikosi cha washika bunduki wa jiji la London kama kocha mkuu amekutana na Guardiola mara mbili akipoteza mechi zote mbili.

Arteta alipoteza kwa 3-0 dimbani Etihad baada ya kurudi kwa EPL mwezi Juni lakini pia alipoteza kwa 2-0 kwenye ligi ya kombe la shirikisho FA.

Kikosi cha Guardiola huenda kikapigwa jeki na kurudi kwa Gabriel Jesus pamoja na Sergio Aguero, ambao wote waili wamerudi mazoezini wiki hii lakini pia huenda Raheem Sterling akapatikana baada ya kujitoa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza baada ya kupata jeraha dogo.

Hata hivyo Kevin De Bruyne huenda akakosekana baada ya kukikacha kikosi cha Ubelgiji kufuatia kupata jeraha waliposhindwa na Uingereza.

Guardiola aidha anatarajiwa kutoa taarifa kamili kuhusiana na swala la viwango wa ‘fitness’ miongoni mwa wachezaji wake.

 

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.