ELUNGATA ANDAA VIKAO VYA USALAMA NA AMANI ENEO LA MADOGO

Mshirikishi mkuu wa utawala kanda ya pwani John Elungata amesema kuwa asasi za usalama zitaendeleza oparesheni ya kudumisha usalama katika kaunti ya Tana River kufuatia uhasama unaoshuhudiwa baina ya jamii ya Orma na  Mnyoyaya.

Haya yanajiri baada ya jumla ya washukiwa  22 kutiwa mbaroni kwa kuhusishwa na mauaji ya watu wawili eneo la Madogo katika kaunti hiyo.

Hata hivyo jamii hizo mbili zimepewa muda wa siku mbili pekee kurudisha mifugo walioibwa ikiwemo mbuzi 48.

Elungata ambaye alizuru kaunti hiyo na kuandaa vikao vya usalama na amani eneo la Madogo kwenye mpaka wa Tana River na Garissa amesema maafisa wa usalama wataendelea kukita kambi hadi pale   hali ya usalama itakaporejea .

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.