Elimu ya mtoto wa kike Kilifi haijakumbatiwa na Jamii hadi sasa

 

Shirika la Action Aid katika kaunti ya Kilifi limesema jamii katika kaunti ya Kilifi imekuwa na dhana potovu kuhusiana na masomo kwa mtoto wa kike.
Akizungumza na meza yetu ya habari Jonathan Kogo wa Shirika hilo amesema bado jamii haijatambua umuhimu wa kumpa elimu mtoto wa kike huku akitaja hali ya umasikini kuchangia katika swala hilo kwani baadhi ya wasichana huajiriwa kama wajakazi ili kukimu mahitaji ya familia zao.
Ameongeza kuwa kufikia sasa idadi kubwa ya wasichana wamejiunga na shirika hilo na kuwataka wazazi kufanya juhudi zao ili kuwarudisha watoto wao shuleni pindi taasisi za elimu zitakapo funguliwa mwakani huku akiwataka kuwa na umakini katika kuwalea watoto hao kama inavyopaswa.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.