Eden Hazard apona jeraha, aanza mazoezi rasmi

Nyota wa Real Madrid, Eden Hazard, ameanza kufanya mazoezi ya uwanjani baada ya kuwa nje kwa muda mrefu akiuguza majeraha. Hazard alianza mazoezi hayo juzi Jumanne akiwa na Marco Asensio ambaye naye alikuwa nje kwa muda mrefu kutokana na majeraha.

Nyota hao walikosa mechi kadhaa za timu hiyo ikiwemo kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, Spanish Super Cup na La Liga.

Wachezaji hao walianza mazoezi huku wakiwa wamevaa viatu maalumu vya kuwazuia wasijitoneshe majeraha yao. Hii ni habari njema kwa kocha wa timu hiyo, Zinedine Zidane hasa kuelekea mechi zao zijazo za Ligi ya Mabingwa Ulaya na La Liga.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.