Droo ya ratiba ya raundi ya 32 ya mitanange ya kombe la FKF Bewtway inatarajiwa kufanywa Ijumaa Februari 19, 2021.
Kwa mjibu wa Shirikisho la Soka (FKF) ni kwamba droo hiyo itafanywa katika jumba la FKF jijini Nairobi kuanzia saa tano asubuhi.
Mechi 32 zilirindimwa kwenye raundi ya 64 wikendi iliyopita huku raundi inayofuata ya 32 ikitazamiwa kuchezwa mwezi April 17 na 18 2021.
Mshindi wa michuano hii ataweka kibindoni kitita cha shilingi milioni 2 sawia na kujikatia tiketi ya kucheza michuano ya kombe la shirikisho Afrika (CAF Confederations Cup).