Dereva wa lori la mizigo amenusurika kifo leo asubuhi baada ya gari lake kutumbukia katika kivuko cha Ferry cha Likoni kaunti ya Mombasa.
Ni mkasa ambao umetokea mwendo wa saa kumi na robo asubuhi baada ya gari hilo kupoteza mwelekeo na kuigonga sehemu ya Ferry ya Mv Kilindini kabla ya kutumbukia baharini.
Ni dereva pekee ambaye alikuwa kwenye lori hilo wakati wa mkasa huo huku shirika la huduma za Ferry nchini ikisema kuwa hali hiyo imetatiza shughuli kwani Ferry hizo zinaegesha kwa matatizo.