CRISTIANO RONALDO SIO MCHEZAJI BORA DUNIANI, GEORGE WEAR

Mshambulizi wa zamani wa klabu ya AC Milan ambaye ni rais wa 25 wa Liberia ambaye ni mchezaji wa zamani wa AC Milan, George Weah,  amesema mcheza soka nguli wa bibi kizee wa Turin, Juventus Cristiano Ronaldo,  siyo mchezaji bora ulimwenguni, lakini anamchukulia Mreno huyo kama kioo kwa wachezaji wachanga.

“Namfananisha Ronaldo na Zlatan Ibrahimovic ambaye kwa sasa wachezaji chipukizi wengi wanajifunza kutoka kwake licha ya umri kumtupa mkono lakini bado anasakata kabumbu kwa kiwango kikubwa,“ amesema Weah.

Weah anaamini Ronaldo kutokana na kujituma kwake bado ataendelea kutikisa ulimwengu wa soka hata kama akifikisha umri wa miaka 40.

CR7 anasherehea siku yake ya kuzaliwa mwezi Februari 26 akiwa anafikisha umri wa miaka 36.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.