Mabingwa watetezi wa ligi Kuu nchini Kenya, KPL, Gor Mahia wametawazwa mabingwa wa msimu 2019/2020.
Gor Mahia imelihifadhi taji hilo baada ya shirikisho la soka nchini FKF kutangaza kukamilika kwa msimu wa ligi kutokana na virusi vya Corona.
Kupitia kwa mtandao wake wa Twitter mwenyekiti wa shirikisho la soka nchini FKF Nick Mwendwa ameipongeza Gor Mahia kwa kushinda ligi na kuongeza kwamba klabu ya City Stars imepandishwa daraja hadi ligi ya KPL.
Ooh and Congratulations Gor Mahia ! You are champions once again and you will represent Kenya on the champions league Next season. Lets do this !
— Nick Mwendwa (@Nmwendwa) April 30, 2020