Chelsea kuwatema Tiemoue Bakayoko, Marcos Alonso, Emerson Palmieri, Michy Batashuayi na David Zappacosta

Klabu ya Chelsea chini ya Kocha mkuu Frank Lampard inapania kupitisha panga la moto kwa wachezaji wake ili kujenga kikosi kipya msimu ujao.

Licha ya hali kuwa tete kiuchumi kutokana na janga la Virusi vya Corona ambavyo vimeivuruga dunia Chelsea inapiga hesabu ndefu za kushusha majembe mapya.

Miongoni mwa majina yanayotajwa sana ni pamoja na Jadon Sancho anayekipiga ndani ya Borussia Dortmund ambaye pia anawindwa na Manchester United.

Majina ya nyota ambao panga linawahusu ni pamoja na Tiemoue Bakayoko anayekipiga Monaco kwa mkopo, Marcos Alonso, Emerson Palmieri, Michy Batashuayi na David Zappacosta.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.