CHANJO YA COVID-19 KUZINDULIWA LEO NCHINI

Huku wizara ya afya nchini ikitarajiwa leo kuzindua utoaji wa chanjo dhidi ya virusi vya corona, waziri wa afya nchini Mutahi Kagwe ametakiwa kueleza wananchi mipangilio kamili kuhusu chanjo hiyo baada ya kubainika kwamba jumla ya shiling bilion 1.65 zitatumika kununua na kuendeleza utoaji wa chanjo hiyo kwa watu million moja.

Mwanaharakati wa maendeleo kutoka ziwa la Ng’ombe kaunti ya Mombasa Ben Oluoch amesema Kagwe anapaswa kueleza kikamilifu  jinsi pesa hizo zitakavyotumika ikizingatiwa kuna kashfa kadhaa zinazozingira wizara ya afya.

Aidha ameihimiza serkali kuifanya chanjo hiyo kuwa ya hiari na kuongeza kwamba iwapo chanjo hiyo italipiwa huenda wengine wakashindwa kutokana na gharama ya juu ya maisha.

 

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.