CHANJO YA ASTRAZENECA YAWASILI NCHINI

Waziri wa afya Mutahi Kagwe amepokea rasmi chanjo ya korona ya Astrazenica katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa JKIA usiku wa kuamkia leo.
Kagwe amesema kuwasilishwa kwa chanjo hiyo ni mojawapo ya hatua kubwa zitakazosaidia katika kukabiliana na janga la Corona.
Waziri huyo amekariri kuwa chanjo hiyo ambayo imehifadhiwa katika chumba maalum kule Kitengela jijini Nairobi itaanza kusambazwa hapo kesho huku wahudumu wa afya wakipewa kipaumbele katika kupokea chanjo hiyo.
Kagwe amesisitiza kuwa chanjo hiyo isiwe sababu ya wakenya kuzembea katika kujikinga dhidi ya korona bali kila mmoja anapaswa kujukumika katika kujilinda.

Kwa upande wake waziri wa uchukuzi James Macharia ambaye aliandamana na Kagwe uwanjani JKIA amesema kuwa chanjo hiyo inatarajiwa kuokoa maisha ya wananchi wengi.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.