Kaunti

Ramadhan Seif Kajembe aaga dunia

 

Aliyekua Mbunge wa Changamwe kaunti ya Mombasa Ramadhan Seif Kajembe ameaga dunia katika Hospitali ya Pandya mjini Mombasa.

Kifo cha Kajembe kinajiri wiki mbili tu baada ya mke wake wa kwanza Aziza Kajembe kufariki kutokana na kile kinachisemekana alikuwa anaugua Covid-19 na Mwezi Machi mwaka huu mke wake wa pili Zaharia Kajembe aliaga dunia.

Mwenda zake Kajembe alihudumu kama mbunge wa Changamwe kati ya mwaka wa 1997 na mwaka 2007 kabla ya nafasi hiyo kuchukuliwa na mbunge wa sasa Omar Mwinyi ambaye alishinda kiti hicho mwaka wa 2013.

Viongozi mbali mbali akiwemo kinara wa chama Cha ODM Raila Odinga kupitia ujumbe wake wa Twitter ni miongoni mwa wale ambao wametuma risala zao za rambi rambi na kumtaja kama kiongozi aliyekuwa amejitolea katika kuwahudumia wenyeji na pia taifa la Kenya kwa ujumla.

Kifo cha Kajembe hakijabainika japo anadaiwa alikuwa na dalili za virusi vya Corona.

Walimu 93 kaunti ya Kwale kupata mafunzo ya masomo mtandaoni

Mwenyekiti wa muungano wa wakuu wa shule za upili nchini KESSHA kaunti ya Kwale Hellen Machuka amesema kwamba shirika la kisayansi na hisabati la SEMESTIER linapania kutoa mafunzo ya masomo ya mtandao kwa walimu 93 kwenye kaunti hiyo kwa muda wa wiki 3 na yatang’oa nanga tarehe 10 mwezi huu wa Agosti .
Machuka amesema ni mafunzo ambayo yatawaelimisha walimu kuhusu masomo ya Mtandao kwani shirika hilo linalenga kuhakikisha walimu wanapata ujuzi wa kuendeleza masomo kwa wanafunzi kupiti mtandaoni.
Hellen Machuka ambaye ni mwalimu mkuu wa shule ya upili ya Matuga amewahimiza wazazi kuwasaidia wanao kupata simu za kisasa ili kuwawezesha masomo yao ili wasisalie nyuma kimasoma.

Irungu Macharia awaonya wahudumu wa magari ya uchukuzi wa umma kaunti ya Lamu

 

Wahudumu wa magari ya uchukuzi wa umma kaunti ya Lamu ambao wanakiuka masharti ya kudhibiti msambao wa virusi vya Corona wameonywa vikali.
Haya ni kulingana na Kamishna wa kaunti hiyo Irungu Macharia ambaye amesema watakaopatikana watapokonywa leseni yao huku akiongeza kuwa msako mkali utaanzishwa na asasi za usalama na wizara ya afya ili kuwachukulia hatua kali wahudumu hao.
Wakati uo huo amesema ni lazima magari hayo kuzingatia masharti ya wizara ya afya kama vile abiria kunawa mikono kabla ya kuabiri magari sambamba na kubeba idadi ya abiria kama inavyopaswa kulingana na serikali ili kuzuia kusambaa kwa virusi hivyo.

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.