Kimataifa

Mchekeshaji Idris Sultan aripoti polisi Dar leo

Mchekeshaji maarufu raia wa Tanzania Idris Sultan leo Ijumaa Novemba 1,  asubuhi ameripoti Kituo cha Polisi ‘Central’ jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya masharti ya dhamana aliyopatiwa jana October 31, 2019.

Sultan alitakiwa kwenda polisi baada ya kuweka picha yenye sura yake huku akiwa ameketi katika kiti chenye nembo ya Taifa na kuambiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuripoti kituo chochote cha Polisi.

Mchekeshaji huyo pia, aliweka picha nyingine inayoonyesha sura ya Rais John Magufuli akiwa amesimama huku amevaa suruali yenye mikanda inayoshikizwa mabegani maarufu kama suspender.

Rais Magufuli alisherehekea siku yake ya kuzaliwa akiwa anafikisha umri wa miaka 60 Jumanne wiki wiki hii.

Muda mfupi baada ya kuchapicha posti yake Sultan, akaunti ya mtandao wa Instagram inayodhaniwa kuwa ya kamishna wa kanda ya Dar es Salaam, Paul Makonda, ilichapisha posti picha moja ya alizoposti Sultan na kuandika akimwambia mchekeshaji huyo ajisalimishe katika kituo cha polisi kilicho karibu naye.

 

Wanaume waliooa waruhusiwa mapadri, Papa atoa idhini

Maaskofu wa kanisa katoliki wamepiga kura kuruhusu wanaume waliooa kuwa mapadri katika eneo moja la pembezoni ili kuweza kupata mwanya wa kuhubiri katika eneo la Amazon.

Hatua hiyo imekuja mara baada ya Papa Francis kutoa ombi kuwa ni vyema kutoa ruhusa kwa wanaume walioa kuwa mapadri kwenye sehemu maalum katika eneo hilola Amazon.

Eneo ambalo waumini wengi wanaotaka kushiriki misa na kupokea mkate wa komunio hawaonagi mapadri kwa zaidi ya miezi kadhaa na muda mwingine hata miaka.

Amesema yeye na washiriki wengine wanaojulikana kama ‘synod’ wapo wazi kwa mawazo ya kutafuta njia mpya itakayosaidia kusambaza imani hiyo.
Watahitajika kupata wanaume wanaoheshimika na kulingana na stakhabadhi hizo watafanya kazi katika jamii wanazotoka.

Maaskofu wa Marekani Kusini wamepigania juhudi hizo ili kukabiliana na upungufu wa mapadri katika eneo hilo. Lakini wakosoaji wamedai kuwa papa anapaswa kuhamasisha mapadri wasioe, ingawaje katika karne ya kwanza ya kanisa, mapadri waliruhusiwa kuoa, na karibia mapapa wote wa mwanzo walikuwa wameoa.

Vilevile kuruhusu wanaume walioa katika sehemu za Amazon ambazo zinakabiliana na ukosefu wa mapadri, kutaenda kinyume na sheria za kikatoliki ambazo zimekuwepo kwa miaka kadhaa sasa.

Kwa sasa papa anaruhusu wanaume walioa kuwa mapadri katika makanisa ya mashariki ya kati pekee.

Botswana kupiga kura leo

Botswana inapiga kura katika uchaguzi mkuu hii leo na kama BBC ilivyogundua katika mjadala iliouandaa hivi karibuni huko Gaborone, Almasi na Tembo au Ndovu wana jukumu kubwa katika kubaini mshindi.

Chama tawala nchini Botswana Democratic Party (BDP) kimeshinda kila uchaguzi nchini Botswana tangu uhuru mnamo 1966, lakini mwaka huu kuna uwezekano hilo likabadilika.

Vyama vitatu ya upinzani vimeungana chini ya Umbrella for Democratic Change (UDC).

Wana manifesto walioinadi kwa makini inayoahidi nafasi laki moja za ajira Katika nchi ambayo zaidi ya 20% ya idadi ya watu hawana ajira.

Mara nyingi Botswana hutajwa kuwa hadithi ya ufanisi Afrika uhuru wake ulipatikana pasi kushuhudiwa umwagikaji damu kama ulivyoshuhudiwa katika maatifa jirani zake, haijawahi kushuhudia vita vya kiraia na mara nyingi uchaguzi mkuu haukumbwi na ghasia.

Sehemu ya utajiri wa Botswana unatokana na almasi. Licha ya kwamba Urusi ina almasi nyingi zaidi kwa jumla, machimbo manne ya madini katika taifa hilo la kusini mwa Afrika lina idadi kubwa ya vito vya thamani duniani na Botswana ina hisa zake katika sekta hiyo ya 50-50 na De Beers, inayojieleza kuwa “kampuni inayoongoza duniani ya almasi”.

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.