Biashara

Uchumi kushuka hadi asilimia 5.4

 

Uchumi wa Kenya huenda ukashuka hadi asilimia 5.4 mwaka huu  kufuatia mlipuko wa virusi vya Corona nchini.

Gavana wa benki kuu ya Kenya Patrick Njoroge amesema namna hali ilivyo kwa sasa uchumi wa Kenya utakuwa wa asilimi 6.2  kwa muda kabla ya kupungua hadi asilimia 5.4.

Amesema biashara ya usafirishaji bidhaa mbali mbali ikiwemo maua imeathirika pakubwa baada ya matifa yanayonunua bidhaa hiyo kufunga mipaka yao.

Amesema japo uchumi utaathirika kwa muda hali itarudi kuwa shwari baada ya janga la virusi vya Corona litakapodhibitiwa na kuwataka wakenya kutohofu lolote kutokana na kushuka kwa uchumi wa taifa kwani mikakati mbali mbali inazidi kuwekezwa kudhibiti hali hiyo na pato la taifa kuimarika.

Deni la nchi latarajiwa kuongezeka mwaka ujao, 2020

Kinara wa chama wa chama cha ANC) Musalia Mudavadi amesema  uchumi wa taifa unazidi kudorora mwaka huu licha serikali kuu kusisitiza kuwa uchumi wa Kenya ulikua kwa asilimia 6 mwaka jana.

Ametaja swala la kukatizwa kwa nafasi za kazi, kampuni kadhaa kukadiria hasara pamoja na kupanda kwa gaharama ya maisha.

Mudavadi anasema hali hiyo inachangiwa na maamuzi mabaya katika jumba la hazina ya kitaifa, mikopo kutoka benki za kibiashara inayotozwa riba ya juu kufadhili kiradi mikubwa mikubwa nchini.

Amesema Kaimu waziri wa fedha Ukur Yattani ana kibarua kikubwa mbele yake katika kutathmini upya deni la Kenya na kusisimua uchumi wa nchi.

Kwa sasa deni la taifa limefikia kima cha shilingi trilioni 6 na linatarajiwa kuongezeka zaidi mwaka ujao kuziba pengo la zaidi ya shilingi bilioni 500 kwenye  bajeti ya mwaka wa 2019/20

Nafasi za ajira zazidi kupungua nchini

Mwaka wa 2019 umekuwa mgumu kwa baadhi ya Wakenya waliopoteza kazi kutokana na hali mbaya ya uchumi iliyosababisha kampuni mbalimbali kusitisha oparesheni zao nchini.

Hata hivyo, baadhi ya waliojikuta katika hali hiyo wamepata njia mbadala za kujikimu.

Kulingana na shirika la takwimu nchini nafasi za kazi zilipungua rasmi kutoka 134,200 mwaka wa 2013 hadi kazi 78,400 mwaka wa 2018 hali hiyo ikishuhudia wakenya wengi kujiajiri kutoka jumla ya kazi elfu 613,250 mwaka wa 2013 hadi laki 8 mwaka 2017.

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.