Michezo

Manchester City waanza kampeni za EPL 2020/21 kwa kishindo, waichapa Wolves 3-1

Mbio za kuwania ubingwa wa kombe la ligi kuu ya Uingereza EPL kwa upande wa klabu ya Manchester City zimeanza kwa mbwembwe baada ya wanaEtihad hao kusajili ushindi wa 3-1 dhidi ya Wolverhampton Wanderers katika dimba la Molineux.

Hii inakuwa mara ya kwanza tangu Januari 2019, kwa Citizens kuchapa Wolves katika mechi yoyote kali baada ya kupoteza nyumbani na mechi za kualikwa katika msimu uliopita.

Wenyeji hao wa Etihad walipata mbinu mpya ya kupambana na mahasidi wao katika mechi yao ya kwanza ya msimu mpya wa 2020-21 na kusajili matokeo ya kuridhisha.

Mabao kutoka kwa Kevin de Bruyne, Phil Foden, na Gabriel Jesus yaliwatosha wageni kuzoa pointi zote katika mechi hiyo. De Bruyne alifunga bao la ushindi katika dakika ya 20 ya mchezo baada ya kuchezewa visivyo na Romain Saiss ndani ya kijisanduku kwa umbali wa yadi 18.

Foden alisawazishia City kunako dakika ya 32 ya mchezo akiwa karibu ya lango na kusaidiwa na Raheem Sterling. Masogora wa Guardiola walitawala mechi hiyo katika awamu ya kwanza na walikuwa na matunda ya kuonyesha juhudi zao.

Upande zote mbili zilirejea kutoka muda wa mapumziko kuendeleza mashambulizi lakini hakuna mmoja kati yao ambaye alifaulu kutingisha wavu hadi dakika ya 78 wakati Raul Jimenez alifungia Wolves bao.

Mchezaji huyo mwenye miaka 29, ambaye ni raia wa Mexico alifunga bao kupitia kichwa kutokea kwa krosi ya Daniel Podence na ilimshinda Ederson Moraes maarifa ya kupangua.

Gabriel Jesus aliweka msumari wa mwisho kwenye jeneza la Wolves katika dakika ya 90 kwa kumalizia vyema baada ya kupiga mpira ndani ya kijisanduku kabla ya kuvurumisha kombora lililotua kimyani.

Mjue Mazinho, baba mzazi wa sajili mpya wa Liverpool, Thiago Alcantara

Jina la Thiago Alcantara limekuwa gumzo siku za hivi karibuni katika dirisha la uhamisho huku vilabu vya EPL vikitafuta huduma zake lakini unajua kwamba hilo sio geni katika familia yao?

Hii hapa ni picha ya baba mzazi wa sajili mpya wa Liverpool Thiago Alcantara do Nascimento iliyopigwa 2013, mzee Ioma do Nascimento maarufu kama, Mazinho. Alikuwa mchezaji kiungo aliyeweza kutoa huduma kama mchezaji Full back.

Alizaliwa katika kijiji cha Santa Rìta, Paraiba nchini Brazil mwaka wa 1966 Aprili 8 na anaurefu wa Mita 1.76 akiwa amewapita wanawe wawili kwa urefu wa Mita 0.02.

Amevitumikia vilabu vingi pamoja na timu ya taifa ya Brazil akicheza jumla ya mechi 371 na kufunga magoli 17 akishinda kombe la Copa America 1989 na kombe la dunia 1994.

Machache yanajulikana kuhusu mkewe, Valeria, ambaye alikuwa mchezaji wa mchezo wa voliboli.

1991 Aprili 11 akiitumikia klabu ya Fiontentina (ambayo imeandikisha ushindi leo katika mechi ya kwanza ya ligi kuu Italia Serie A kwa kuichapa Torino 1-0) nchini Italia, Mazinho alibarikiwa na mtoto na kumpa jina la Thiago asijue atakuja kuwa zaidi ya yeye katika ulingo wa mchezo wa soka.

Miaka miwili baadaye (1993) Mazinho alibarikiwa na mtoto wa pili akiwa na klabu ya nyumbani Brazil inayofahamika kwa jina la Palmeiras, na kumpa jina la Rafael ambaye ninavyoandika hii blogu anaitumikia timu ya taifa ya Brazil na klabu ya Celta Vigo kwa mkopo akitokea Barcelona. Wengi wanamjua mchezaji huyu kama Rafinha ambaye ni mwiba kweli kweli.

Mwanawe Mazinho, Thiago Alcantara anauraia wa mara tatu. Yeye ni mzawa wa Italia, lakini babake ni raia wa Brazil huku yeye mwenyewe akiwa na uraia wa Uhispania ambako anaitumikia timu ya taifa.

Endapo nyota ya Thiago itazidi kung’aa furaha ya Mazinho itazidi lakini hata nyota ikifeli bado yuko Rafinha ambaye huenda akaja kuwa mwiba zaidi ya wanafamilia wote hususan kwenye ulingo wa mchezo wa soka.

Kombe la Carabao | Bournemouth uso kwa uso na Manchester City

Sasa ni rasmi kwamba klabu ya Bournemouth watamenyana na Manchester City kwenye kivumbi cha kombe la Carabao baada ya kuwalaza Crystal Palace 11-10 kupitia mikwaju ya penalti kwenye raundi ya pili ya kipute hicho kufuatia ya kuambulia sare tasa mwishoni mwa dakika 90.

Ushindi wa Bournemouth uliwakatia tiketi ya kuchuana sasa na mabingwa watetezi Manchester City kwenye raundi ya tatu wiki ijayo.

Baada ya wachezaji wote 20 (isipokuwa makipa), kufunga penalti zao, mlinda-lango Wayne Hennessey aliudaka mkwaju wa kipa Asmir Begovic wa Bournemouth kabla yay eye mwenyewe kuupaisha mkwaju wake juu ya mlingoti.

David Brooks alifunga mkwaju wake wa pili wakati wa kuchanjwa kwa penalti huku Begovic akipangua kombora la Luka Milivojevic kwa upande wa Bournemouth na kuwapa fursa ya kusonga mbele.

Bournemouth walitamalaki mchezo, wakawazidi maarifa wapinzani wao katika takriban kila idara na kuwaelekezea makombora 17 yaliyolenga shabaha. Palace walifanya majaribio manne pekee langoni pa Bournemouth walioshushwa daraja kwenye Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) mwishoni mwa msimu wa 2019-20 baada ya kipindi cha miaka mitano.

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.