Business

Miundo msingi yatajwa kuchangia kuboreka kwa sekta ya utalii kanda ya pwani.

Huduma za uchukuzi kupitia kwa reli ya kisasa,SGR zimetajwa kuwa na manufaa tele katika wizara ya utalii mkoa wa pwani.

Kutokana na uchukuzi huo shughuli za kibiashara zimeboreka kwa kiwango kikubwa hasa katika sekta ya mikahawa na hoteli.

Kuimarika kwa hali ya miundo msingi pia kumetajwa kuchangia kuboreka kwa sekta ya utalii huku watalii wa hapa nchini wakifurika Pwani ili kusherehekea likizo ya Pasaka.

Kwa sasa, sekta ya mahoteli inashuhudia asilimia 100 ya wageni, asilimia 90 wakiwa wageni kutoka Kenya na asilimia 10 wa kimataifa.

Benki ya Equity kuwekeza nchini Ethiopia

Benki ya Equity inapania kuwekeza katika taifa la Ethiopia ikiwa ni kati ya mpango yake ya kuwa benki ya bara la Afrika.

Kwa mujibu wa Mkurungezi mkuu wa benki hiyo James Mwangi kwa sasa benki hiyo ina mtaji wa dola bilioni 1.3 na tayari imeanza upya harakati za upanuzi katika bara la Afrika.

Mwangi amesema benki hiyo inafuatilia sera za mageuzi katika taifa la Ethiopia na iko kwenye mikakati ya kuanza oparesheni nchini humo.

Kwa sasa nchi ya Ethiopia ina takribani benki 18 za kibiashara huku serikali ikimiliki Commercial Bank of Ethiopia pamoja na ile ya Maendeleo.

 

Uhaba wa mafuta ya petroli washuhudiwa kaunti ya Tana River

Wahuhumu wa boda boda katika kaunti ya Tana River wanasema bishara zao zimeathirika kwa kiwango kikubwa kutokana na uhaba wa mafuta ya petroli katika vituo vya kuuzia mafuta kwenye kaunti hiyo.

Hali hiyo imewalazimu abiria kuingia zaidi mfukoni baada ya wahudumu hao kuongeza nauli kutoka shilingi hamsini hadi shilingi mia moja.

Wanalazimika kutafuta mafuta ya petroli katika miji ya Garisa na Masalani kwenye kaunti ya Garisa ili kuendeleza biashara zao.

Inadaiwa kuwa baadhi ya wenyeji wa kaunti ya Tana River wamekuwa wakinunua mafuta hayo kwa wingi eneo la Ijara kaunti ya Garisa na kuwauzia wahudumu wa boda boda kwa bei ya reja reja huku chupa ya nusu lita ya mafuta hayo ikiuzwa kwa shilingi 100.

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.