Carabao | Liverpool na Man United wajiunga na Man City, wafuzu robo fainali

Mshambuliaji wa Manchester United Marcus Rashford, amefunga mabao mawili muhimu yalioivusha timu yake kwenye hatua ya Robo Fainali ya Carabao Cup.

United ilikuwa inamenyana na Chelsea ambapo mchezo ulikuwa na ushindani mkali na mwisho wa dakika 90 Manchester ilishinda mabao 2-1.

Rashford alianza kucheka na nyavu dakika ya 23 kwa penalti kabla ya Mitch Batshuayi kusawazisha dakika ya 61 na bao la ushindi kwa United likafungwa dakika ya 73 kwa mpira uliovurumishwa na Rashford na kuzama mzima nyavuni katika uwanja wa Stamford Bridge.

Na kwa upande wa Liverpool kikosi hicho kimesonga hatua ya Robo Fainali ya Carabao Cup baada ya ushindi wa penalti 5-4.

Mchezo huu ambao umechezwa uwanja wa Anfield ulikuwa na maajabu yake kwani ulikusanya jumla ya mabao 10 ndani ya dakika 90.

Sare ya mabao 5-5 ilipelekea timu hizo kupigiana penalti ambapo Arsenal ilishinda penalti 4 na kukosa moja huku Lierpool ikishinda penalti zote tano.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.