Bunge la kitaifa kutumia lugha ya Kitaifa kwenye vikao vyake

Vikao vya kamati ya bunge la kitaifa vitakuwa sasa vikitumia lugha ya Kiswahili kwenye mijadala na ripoti zake.

Hii ni baada ya spika wa bunge la kitaifa ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai kuzindua rasmi mpango huo na kupongeza hatua ya bunge la Kenya kwa kuzindua lugha hiyo ambayo itakuwa ikitumika kwenye vikao mbali mbali ya bunge na kupeperushwa moja kwa moja kwenye vyombo vya habari tofauti na ilivyokuwa hapo awali.

Kulingana na Ndugai ni kuwa mataifa mengi ya Afrika yanapaswa kutumia lugha ya Kiswahili kwani wananchi wataweza kufahamu mambo ambayo yanatekelezwa na wabunge katika kuwafanyia maendeleo.

Ni hatua ambayo imeungwa mkono na spika wa bunge la Kitaifa Justine Muturi akisema itakuwa bora kwa kuwa ripoti sambamba na vikao bungeni vimekuwa vikiandikwa na kujadiliwa kwa lugha ya kingereza huku aliyekuwa spika wa zamani katika bunge la Kitaifa Francis Ole Kaparo akihoji itawasaidia wananchi kufahamu maswala ambayo huwa yanaendelezwa kwenye bunge.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.