Bunge la kaunti Kilifi lapitisha mswada kuzisaidia vilabu vya mpira kifedha

Bunge la kaunti ya kilifi imepitisha mswada utakaoona timu za eneo hili zikipata ufadhili siku chache baada ya timu ya Kilifi all stars kutemwa nje ya michuano ya divishen one kwa kukosa kucheza mechi tatu mfululizo.

Akiongea na Tama la Spoti mwakilishi wadi wa wadi ya Kakuyuni Nixon Mramba ambaye ndiye aliyewasilisha mswada huo bungeni, ni kwamba changamoto ambazo timu zinapitia kifedha ni nyingi jambo lililopelekea kuunda mswada huo kuzisaidia.

”Nimepata changamoto nyingi sana kutoka kwa timu zetu ambazo zinashiriki ligi ya kaunti kwenda juu na hata timu ambayo tulikuwa tumeitegemea kwenye michuano ya daraja la kwanza, Kilifi All Stars, ilishushwa daraja hadi daraja la pili kwa sababu ya kukosa kucheza michezo mitatu kufuatia kukosa usafiri. Nilikutana na mwenyekiti wa FKF tawi la malindi Dickson Muramba na akanielezea changamoto nyingine nyingi zaidi ndio nikaamua kupeleka mswaada wa kuzisaidia timu hizi na jana Jumanne mswada huu ulipitishwa,” amesema Mramba.

Mramba aidha amesema kwamba ufadhili huu utatia motisha vijana kujihusisha na michezo na kuachana na matumizi ya dawa za kulevya pamoja na kupunguza visa vya mimba za utotoni.

Ameongeza kwamba wizara ya michezo kaunti ya Kilifi haikuwa na mipango maalum ya kuzisaidia timu za eneo la Kilifi ila kwa kupitisha mswada huu pamoja na kusukuma utekelezwaji wake talanta miongoni mwa vijana zitakuzwa vyema.

 

 

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.