Botswana kupiga kura leo

Botswana inapiga kura katika uchaguzi mkuu hii leo na kama BBC ilivyogundua katika mjadala iliouandaa hivi karibuni huko Gaborone, Almasi na Tembo au Ndovu wana jukumu kubwa katika kubaini mshindi.

Chama tawala nchini Botswana Democratic Party (BDP) kimeshinda kila uchaguzi nchini Botswana tangu uhuru mnamo 1966, lakini mwaka huu kuna uwezekano hilo likabadilika.

Vyama vitatu ya upinzani vimeungana chini ya Umbrella for Democratic Change (UDC).

Wana manifesto walioinadi kwa makini inayoahidi nafasi laki moja za ajira Katika nchi ambayo zaidi ya 20% ya idadi ya watu hawana ajira.

Mara nyingi Botswana hutajwa kuwa hadithi ya ufanisi Afrika uhuru wake ulipatikana pasi kushuhudiwa umwagikaji damu kama ulivyoshuhudiwa katika maatifa jirani zake, haijawahi kushuhudia vita vya kiraia na mara nyingi uchaguzi mkuu haukumbwi na ghasia.

Sehemu ya utajiri wa Botswana unatokana na almasi. Licha ya kwamba Urusi ina almasi nyingi zaidi kwa jumla, machimbo manne ya madini katika taifa hilo la kusini mwa Afrika lina idadi kubwa ya vito vya thamani duniani na Botswana ina hisa zake katika sekta hiyo ya 50-50 na De Beers, inayojieleza kuwa “kampuni inayoongoza duniani ya almasi”.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.