Bei ya unga wa mahindi nchini yatarajiwa kupanda hata zaidi

Wakenya wanaendelea kuhimizwa kujitayarisha kwa kipindi kigumu cha maisha na bei ya bidhaa ikitrajiwa kupanda bei maradufu baada ya ongezeko la bei ya mafuta nchini.

Wadau katika sekta ya kilimo wanasema hali ya kupanda kwa gharama ya maisha inatarajiwa kuzidi kushuhudiwa katika miezi ijayo na bei ya unga wa mahindi nayo ikisemekana huenda ikapanda bei hata zaidi kuliko ilivyo kwa sasa.

Ingawa serikali imesisitiza kuwa nchi ina mahindi ya kutosha ambayo yamehifadhiwa na kuwatosheleza wananchi hadi mwezi Julai ukosefu wa mvua na kiangazi cha muda mrefu kumechangia kwa hali ya maisha kuwa ngumu.

Waziri wa kilimo Mwangi Kiunjuri anasema kuwa nchi ina jumla ya magunia milioni 21.3 kutoka kwa wakulima, wafanyabiashara, wasindikaji na Bodi ya Taifa ya nafaka na mazao nchini NCPB.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.