Baraza la mashauri ya kiislamu nchini KEMNAC limeendelea kutoa shinikizo kuwa mchakato wa BBI ndio suluhu tosha la uongozi nchini.
Mwenyekiti wa baraza hilo, Sheikh Juma Ngao amewataka wakaazi wa pwani kuunga mkono ripoti hiyo ya BBI ilikufanikisha uongozi kupitia mifumo itakayowanufaisha wakenya kupitia mageuzi maalum.
Sheikh Ngao amesema kuwa mabadiliko ya uongozi ni sharti ya fanikishwe na hilo litafaulu kupitia mchakato wa BBI.
Kiongozi huyo amewataka viongozi kukoma kuzozana na badala yake waungane na kuhakikisha kuwa wanawafanyia maendeleo wakaazi badala ya kuendekeza siasa.