Viongozi mbali mbali katika kaunti ya Kilifi wanaendelea kujiweka kwenye karantini baada ya kutangamana na naibu wa gavana wa kaunti ya Kilifi Gedeon Sabari ambaye alipatikana na virusi vya Corona baada ya kurejea nchini Kutoka Ujerumani.
Baadhi ya viongozi hao ni mwakilishi wa kina mama Getrude Mbeyu, mbunge wa Ganze Teddy Mwambire, William Kamoti ambaye ni mbunge wa Rabai sambamba na katibu msimamizi katika wizara ya ardhi Gedion Mung’aro.
Ikumbukwe waziri wa afya nchini Mutahi Kagwe alisema naibu gavana wa kaunti ya Kilifi Gedeon Saburi atafunguliwa mashtaka baada ya kipindi cha Karantini kukamilika kwa kuhatarisha maisha ya wakenya baada ya kufanya mikutano na kutangama nao baada ya kuejea Kenya kutoka Berlin Ujerumani.