Baada ya miaka 15 ya ujane, mtangazaji Isabella ampata mme

Baada ya miaka 15 ya kuwa nje ya ndoa kufuatia kuaga dunia kwa mme wake, mtangazaji wa runinga humu nchini, Isabella Kituri, ametangaza kuolewa tena.

Akiwa mwingi wa furaha, Isabella alichapisha mitandaoni picha ya mumewe akiwa amembeba mtoto wao na kumshukuru kwa kumuandalia sherehe hiyo.

Ndoa ya kwanza ya Isabella ilidumu kwa mwaka mmoja na ikabarikiwa na mtoto mmoja kabla ya bwanake kuaga dunia mwaka wa 2005 baada ya kuugua kwa muda mrefu kutokana na saratani ya utumbo.

Wakati mme wa mtangazaji huyo akiaga dunia mtoto alikuwa na umri wa miezi mitatu na Isabella alilazimika kumlea mwanawe akiwa mpweke huku mchungaji wake akiwa kwenye mstari wa kumshauri na kumtia moyo kipindi hicho kigumu.

Isabellah alijifungua mtoto wake wa pili mwaka wa 2019 ambapo mashabiki wake walimpongeza na kumtakia malaika huyo heri njema. na maisha marefu yenye fanaka.

 

 

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.