BAADA YA DHIKI CHELSEA YATIA GUU MOJA SEMI FAINALI

Vijana wa Kocha mjerumani Thomas Tuchel Chelsea hapo jana walijifariji na ushindi wa raundi ya kwanza ya mitanange ya mabingwa ulaya UEFA dhidi ya Fc Porto.

Muingereza Mason Mount na mlinzi Benjamin Chillwell ndio waliotinga magoli hayo hapo jana ambayo yatawafaa hasa ikiwa ni ushindi wa ugenini. Mtanage huo wa hapo jana sawia na ule wa marudiano ya raundi ya pili wa robo fainali utafanyika katika uga wa Estadio Ramon Sanchez (Sevilla) kwa sababu ya masharti yaliyowekwa na serikali za Uingereza na Ureno kutoruhusu usafiri wa kigeni kama njia moja wapo ya kudhibiti msambao wa virusi vya corona.

Chelsea wikendi iliyopita walititigwa mabao 5-2 na Westbrom katika mtanange wa ligi kuu ya Uingereza EPL ambayo ilikuwa mechi ya kwanza kwa mkufunzi huyu mpya wa Chelsea Tuchel kupoteza tangu ujio wake.

Na kwengineko miamba wa ligi kuu ya mabingwa ulaya (UEFA) Bayern Munich ambao pia ni mabingwa watetezi wa kombe hilo walirambishwa sakafu hapo jana na wapinzani wao wa fainali ya msimu uliopita Paris Saint Germain mabao 3-2 ugani Allianz Arena huko Munich. Mabao ya Kylian Mbappe na Marquinhos ndio yaiyowapa wafaransa hao ushindi wa ugenini.

Hata hivyo Choupo-Moting naThomas Muller ndio walioifungia Bayern katika mechi hiyo. Mshambulizi Robert Lewandoski alikosekana katika mtanange huo hapo jana baada ya kupata jeraha katika mechi ya hapo awali.

Hii leo mechi za raundi ya kwanza za robo fainali za Europa zitakuwa zinarindimwa usiku wa leo ambapo Ajax watakuwa wanavaana AS Roma, Arsenal watapimana nguvu na Slavia Prague, D.

Zagreb nao kulicheza dhidi ya Villarreal na hatimaye mashetani wekundu Manchester United watakuwa wageni wa Granada CF huko Uhispania

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.