Awamu ya kwanza ya ugavi wa chakula cha msaada yatamatika Mombasa

 

Shirika la msalaba mwekundu katika kaunti ya Mombasa limefaulu kumaliza awamu ya kwanza ya ugavi wa chakula kwa wale walio lengwa katika mradi huo.
Akizungumza mjini Mombasa mwenyekiti wa shirika hilo Mohamoud Noor amesema kuwa lengo lao ni kufikia nyumba laki mbili na ishirini na saba na kwa sasa tayari wamefikia watu zaidi ya elfu thelathini na tano katika kaunti ndogo ya Mvita huku wakitarajia kukamilisha ugavi huo katika kaunti ndogo ya likoni na kisauni
Hata hivyo Mahamood amedhibitisha kuwepo kwa visa vya udanganyifu katika shughuli hiyo na kuelezea kisa cha maafisa wa nyanjani kuwa na upendeleo kwa baadhi ya familia katika eneo hilo nakusema kuwa tayari wameshughulikia visa hivyo vilivyo kwani vilikuwa visa kidogo ikilenganishwa jumla ya shughuli yote
Aidha mwenyekiti huyo ametaja hatua ya watu kufutwa kazi kama changamoto kubwa kwani wanadai kuwa waathirika wa janga la corona na kuwa wanahitaji kupewa msaada huo wa chakula.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.