By Janet Mumbi

Wakili Nelson Harvey ndiye mwenyekiti wa LSK

 

Wakili Nelson Harvey ndiye mwenyekiti wa LSK baada ya  kuibuka mshindi katika uchaguzi uliofanywa hapo jana.
Harvey aliibuka mshindi baada ya kuwapiku mawakili Charles Kanjama, Maria Mbeneka sambamba na Maria Chigai ambao pia walikuwa wanagombea wadhfa huo.
Harvey sasa ndiye mwenyekiti mpya baada ya aliyekuwa mwenyekiti Alen Gichuhi.

 

Katibu wa chama cha kutetea maslahi ya walimu nchini (KNUT) tawi la Malindi na Magarini kaunti ya Kilifi Fredrick Nguma, amezungumzia swala la kupunguzwa kwa alama za kujiunga na shule ya mafunzo ya walimu katika vyuo vikuu nchini.
Nguma amesema kuwa mfumo huo umekua ukitumika hapo awali na kuwafaidi walimu wengi katika taifa hili na kuongeza kuwa ipo haja ya kutekelezwa kwa swala hilo hasa katika maeneo ya kaskazini mashariki mwa nchi kutokana na uhaba wa walimu ambao umekuwa ukishuhudiwa eneo hilo.
Akizungumzia mchakato wa BBI amesema KNUT itaunga mkono mapendekezo hayo kiukamilifu ili kupata fursa ya kuwachagua makamishna wao kwa njia ya kupiga kura.
Aidha ametoa mwito wa walimu kutokihama chama hicho licha ya changamoto zilizoko kwani imekuwa ikiwatetea walimu tangu mwaka wa 1946 ili maslahi yao yatekelezwa kama inavyopaswa.

Huduma za maji zarejea Kwale

Gavana wa kaunti ya Kwale Salim Mvurya amesema huduma za maji katika eneo hilo zitaanza kurejea katika hali yake ya kawaida.
Hii ni baada ya wenyeji kushuhudia uhaba wa maji kwa taktibani wiki tatu huku Gavana huyo akisema hali hiyo ilichangiwa na hitilafu za kimitambo katika kituo cha kusambaza maji cha chemi chemi za maji cha Mwarere.
Amesema kutokana na changamoto za maji ambazo zimekuwa zikiikabili kaunti hiyo sasa wanashirikiana na bodi ya kitaifa ya kudhibiti maji kuhakikisha hali hiyo inapata suluhu la kudumu ili kuwaepusha wenyeji dhidi ya kukumbwa na tatizo hilo.

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.