ASILIMIA KUBWA YA WANAFUNZI KAUNTI YA KWALE WAMERIPOTI SHULENI

Wazazi ambao wanawaficha watoto wao wa kike waliopata ujauzito badala ya kuwapeleka shuleni ili kuendeleza masomo yao katika eneo bunge la Msambweni wameonywa vikali na maafisa tawala katika kaunti ya Kwale.

Wakiongozwa na Chifu wa Kinondo Mohamed Mwatajiri amehoji kuwa wazazi hao wanapaswa kushirikiana na maafisa hao tawala ili kuhakikisha wanafunzi wote wanarudi shuleni.

Mwatajiri ameongeza kuwa tangu kufunguliwa kwa shule zote kote nchini mapema mwezi huu wa Januari ni kuwa asilimia 94 ya wanafunzi wa shule za msingi eneo hilo wameripoti shuleni huku shule za upili zikirekodi asilimia 89 ya wanafunzi.

 

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.