Arsenal yamuuza nahodha wao Laurent Koscielny

Arsenal wamemuuza beki wao wa kati na nahodha Laurent Koscielny kwa klabu ya Bordeaux kwa dau la Euro milioni 5. Mchezaji huyo mwenye miaka 33 anarejea katika ligi ya Ufaransa baada ya miaka tisa ya kucheza Uingereza katika klabu ya Arsenal.

Koscielny alikuwa amebakiza mwaka mmoja kwenye mkataba wake na Arsenal na klabu hiyo yenye maskani yake jijini London ilitaka mchezaji huyo aendelee kusalia klabuni hapo.

Hata hivyo, mchezaji huyo aling’ang’ania kuuzwa na kugoma kusafiri na timu kwenda kwenye ziara ya kujiandaa na msimu mpya nchini Marekani. Naye mshambuliaji wa Manchester United, Romelu Lukaku atapewa adhabu na klabu yake kwa kukosa mazoezi bila ruhusa.

Nyota huyo wa timu ya Taifa ya Ubelgiji mwenye umri wa miaka 26, amekuwa akifanya mazoezi na timu yake ya zamani Anderlecht kwa muda wa siku mbili zilizopita.

Timu ambazo zinashiriki Serie A, Inter Milan na Juventus zinapigana vikumbo kupata saini ya nyota huyo ambaye hajacheza mechi za maandalizi kutokana na kusumbuliwa na majeraha. Julai, United ilipiga chini dau la pauni milioni 54 kutoka Inter Milan kwa ajili ya kumpata nyota huyo.

Lukaku alijiunga na United msimu wa mwaka 2017 akitokea Everton kwa dau la pauni milioni 75 msimu uliopita alitupia mabao 12.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.