AISHA JUMWA AMTAKA GAVANA KINGI KUHAKIKISHA WENYEJI WA KILIFI WANAPATA NAKALA ZA BBI

Mbunge wa Malindi kaunti ya Kilifi Aisha Jumwa amemtaka gavana wa kaunti ya Kilifi Amason Jeffa Kingi kuhakikisha kuwa wakaazi wanapatiwa nakala za BBI wajisomee kabla ya kufanya uamuzi wa aina yoyote.
Akihutubia wananchi katika hafla ya kuadhimisha tamasha la tamaduni za Kimijikenda katika eneo bunge la Malindi Kaunti ya Kilifi Jumwa amesema kuwa ni sharti gavana Kingi achukue jukumu la kuwapatia wananchi hao ripoti hiyo badala ya wao kushurutishwa na viongozi kuweka sahihi pasi na kuelewa kilichomo.
Jumwa ameongeza kuwa iwapo wananchi wa Kaunti ya Kilifi hawatapata fursa ya kusoma mapendekezo ya ripoti ya BBI basi ni wazi kuwa hawatachukua hatua yoyote ya kuweka sahihi zao.
Aidha kiongozi huyo amewatahadharisha wakaazi wa eneo hili dhidi ya kuweka sahihi zao kwa kile alichosema kuwa huenda wakaharibikiwa katika maswala mbalimbali hivyo kuna haja ya wo kuelewa kilichomo ndani ya BBi kabla ya kuweka sahihi.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.