AISHA JUMWA AITAKA SERIKALI YA KAUNTI YA KILIFI KUGHARAMIA MATIBABU YA MAJERUHI WALIOLAZWA KUFUATIA AJALI

Mbunge wa Malindi kaunti ya Kilifi, Aisha Jumwa ameitaka serikali ya kaunti ya Kilifi kuzisaidia kwa gharama za mazishi jamii zilizopoteza wapendwa wao katika ajali mbaya ya barabarani iliyofanyika jana kule Kizingo,Gede kwenye barabara kuu ya Malindi- Mombasa.

Akizungumza na wanahabari katika hospitali ya rufaa ya kaunti ndogo ya Malindi, Jumwa amesema kuna haja ya serikali kusimamia malipo yanayotozwa kupata huduma za kuhifadhia maiti huku pia akiitaka serikali kugharamia matibabu ya majeruhi wote waliolazwa katika hospitali hiyo.

Jumwa amesema kuwa iwapo serikali ya kaunti haitajukumika katika swala hilo basi atahakikisha kuwa jamii zilizokumbwa na msiba sawia na zile ambazo wapendwa wao wamejeruhiwa zinapata msaada.

Ni ajali ambao ilipelekea baadhi ya jamii kukumbwa na majonzi baada ya kuwapoteza wapendwa wao waliokuwa tegemeo kwao huku idara ya usalama ikithibithisha kufariki kwa watu 15.

 

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.