Agizo la kudumisha usafi laendelea kuzingatiwa na wenyeji wa lamu

Wenyeji katika kaunti ya Lamu wanaendelea kuzingatia agizo la serikali kupitia wizara ya afya ya kudumisha usafi kama njia moja ya kudhibiti maambukizi ya virusi vya Corona.
Wanasema kuwa kando na serikali ya kaunti hiyo kuweka maji na sabuni katika maeneo ya umma ili kunawa mikono sasa wenyeji hao wametoa wito kwa serikali kuwapa vieuzi katika makazi yao ili kuzuia maambukizi ya virusi hivyo.
Aidha, wameitaka serikali hiyo kutoa hamasa kwa wakazi namna ya kujikinga dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona.
Hata hivyo wenyeji hao wamehimizwa kuzingatia swala la usafi ili kujikinga dhidi ya maambukizi hayo.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.