Abdalla Fadhil amtaka Rais Uhuru Kenyatta kuwatimua viongozi ambao ni wafisadi

 

Baadhi ya viongozi katika kaunti ya Lamu wanatoa wito kwa serikali kuwatimua viongozi ambao ni wafisadi wakati huu taifa linapoendeleza harakati za kukabiliana na janga la Corona.
Viongozi hao wakiongozwa na Abdalla Fadhil ambaye anashughulika na maswala ya kijamii nchini wanamtaka rais Uhuru Kenyatta kulegeza kamba ya kuabudu wakati huu Waislamu wako kwenye mfungo wa Ramadhani.
Fadhil amesema itakuwa vyema ikiwa watafanya mkutano na maafisa katika idara ya afya ili kuafikiana kuhusu kufunguliwa kwa nyumba za ibada kwa kupewa masharti ya kuzingatia ili kujilinda dhidi ya Corona.
Amewaomba wanaohusika katika ugavi wa chakula cha msaada kwa jamii zisizojiweza kujukumika kuhakikisha wanawafikia walengwa.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.