KINARA WA ODM RAILA ODINGA AWATAKA WANASIASA KUTO KIUKA SHERIA ZA VYAMA VYAO

Kinara wa chama cha ODM,Raila Odinga amesema kuwa kuna haja ya wanasiasa kuwajibika katika kupiga siasa zao pasi na kukiuka sheria za vyama wanavyovitumia kuwania nyadhfa mbalimbali.

Odinga amesema kuwa iwapo kiongozi yoyote anatofautiana na uongozi wa chama ni sharti kiongozi huyo ajiuzulu sambamba na kufuatia sheria hitajika ili kujitoa katika chama husika badala ya kukashifu mifumo ya wanachama au uongozi wa chama hicho.

Odinga ametaja baadhi ya viongozi kuendekeza siasa za kinafiki kwa kukiuka sheria za vyama na badala yake kuzungumza vibaya kuhusu vyama hivyo.

Akirejelea tukio ambapo alilazimika kujitenga na chama alichokuwa ndani hapo awali,Odinga amesema kuwa alifuata taratibu zilizohitajika ili kujitoa katika chama hicho mwaka 1997.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.