kilifi yatajwa kama mojawepo ya maeneo ambayo huenda yakaathirika zaidi na ugonjwa wa corona

Zaidi ya wafanyikazi 100 wa kaunti ya Kilifi wakiongozwa na gavana Amason Kingi wanaendelea kujitenga kwa kipindi cha siku 14 wakizingatia hali yao ya afya baada ya kutangamana kwa karibu na naibu gavana wa kaunti hiyo Gideon Saburi.
Haya yanajiri huku kaunti ya kilifi ikitajwa kama mojawepo ya maeneo ambayo huenda yakaathirika zaidi na ugonjwa wa corona.
Kulingana na taarifa ni kuwa Saburi alipowasili nchini alihudhuria hafla 3 za mazishi, maeneo ya burudani na hata kwenye ofisi za kaunti bila kujitenga huku Kingi akihofia walioambukizwa na Saburi huenda wakawa wengi zaidi katika kaunti hii ya Kilifi wakiwemo watu waliokutana nao katika vilabu ya burudani maeneo ya Nyali, Bamburi na Mtwapa.
Saburi pamoja na dereva wake wanaendelea kutibiwa katika hospitali ya Mbagathi jijini Nairobi huku waliotangamana naye wakiendelea kutafutwa.
Siku ya Jumanne  waziri wa afya nchini Mutahi Kagwe alisema kaunti zilizoathirika zaidi ni Nairobi, Mombasa, Kilifi, na Kwale.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.