Katibu wa chama cha kutetea maslahi ya walimu nchini (KNUT) tawi la Malindi na Magarini kaunti ya Kilifi Fredrick Nguma, amezungumzia swala la kupunguzwa kwa alama za kujiunga na shule ya mafunzo ya walimu katika vyuo vikuu nchini.
Nguma amesema kuwa mfumo huo umekua ukitumika hapo awali na kuwafaidi walimu wengi katika taifa hili na kuongeza kuwa ipo haja ya kutekelezwa kwa swala hilo hasa katika maeneo ya kaskazini mashariki mwa nchi kutokana na uhaba wa walimu ambao umekuwa ukishuhudiwa eneo hilo.
Akizungumzia mchakato wa BBI amesema KNUT itaunga mkono mapendekezo hayo kiukamilifu ili kupata fursa ya kuwachagua makamishna wao kwa njia ya kupiga kura.
Aidha ametoa mwito wa walimu kutokihama chama hicho licha ya changamoto zilizoko kwani imekuwa ikiwatetea walimu tangu mwaka wa 1946 ili maslahi yao yatekelezwa kama inavyopaswa.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.